Viongozi wa Africa na wa ulimwengu wote wanakubaliana juu ya hatua thabiti kusukuma ukuaji wa kilimo barani Afrika

By The African Green Revolution Forum (AGRF)
Viongozi wa Africa na wa ulimwengu wote wanakubaliana juu ya hatua thabiti kusukuma ukuaji wa kilimo barani Afrika
Viongozi wa Africa na wa ulimwengu wote wanakubaliana juu ya hatua thabiti kusukuma ukuaji wa kilimo barani Afrika

ARUSHA, Tanzania, October 1, 2012/African Press Organization (APO)/ -- Baraza la Uboreshaji wa Kilimo Afrika (The African Green Revolution Forum (AGRF)) (http://www.agrforum.com) lililohitimishwa leo mjini Arusha, lilitoa hatua thabiti za kubadilisha sekta ya kilimo ya Afrika. Wakuu wa nchi za Afrika, mawaziri, wawakilishi wa sekta ya kibinafsi, jumuiya ya kimataifa na wakulima waliungana katika mpango wa kuongeza mazao ya kilimo na ukuaji wa mapato wa sekta ya kilimo ya Afrika. Ufadhili wa wakulima wadogo wa Afrika bado ndilo suluhisho kuu zaidi.


Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/agrf.jpg


Akitoa kauli juu ya ufanisi wa baraza hili na hatua muhimu zitakazofuata, Raisi wa Mwungano wa Uboreshaji wa Kilimo (Alliance for a Green Revolution (AGRA)), na mwenyekiti mwenza wa baraza hilo, Jane Karuku alisema, “Jumuiya ya kimataifa inaanza kutambua kwamba wakulima wadogo ni wawekezaji, na kilimo ni biashara. AGRF liliamsha majadiliano makubwa sana na kutoa mipango inayoweza kutekelezeka ili itufikishe karibu na kupata usalama wa chakula na lishe bora. Ni muhimu sana kwamba tusonge mbele na hatua hizi halisi, za utendaji na za vitendo katika daraja la mkulima, na sio katika daraja la ofisini.”


“Baraza linafanya kazi kama kiangulio muhimu kwa ajili ya kutoa suluhisho vumbuzi za kukuza sekta ya kilimo ya Afrika,” alisema Raisi na Mkurugenzi Mkuu wa Yara, na mwenyekiti mwenza wa hilo baraza Bw. Jørgen Ole Haslestad. “Kwa kukusanya viongozi wa sekta ya uma- na sekta ya kibinafsi ili washirikiane kati ya nchi na tasnia, tuna matumaini mazuri kwamba matokeo ya mwisho yatakuwa ongezeko la usalama wa chakula katika siku za usoni.”


Maeneo ya hatua za AGRF yaliweka msisitizo juu ya dhamira nne kuu: kufikiria upya juu ya ushirika kati ya sekta za uma na za kibinafsi, kufanya mageuzi katika fedha za kilimo, kufanya masoko yafanye kazi, na kujenga misingi ya ukuaji wa haraka katika uzalishaji wa kilimo. Mifano ya hatua maalum zilizoamuliwa kwa pamoja ni pamoja na:


• Fedha za kushawishi na kuchochea:Kuendeleza miundo ya kuchochea taasisi za kifedha zikopeshe/ziwekeze katika kilimo, hasa katikati ya wakulima wadogo maskini, na waliotengwa na jamii; na kuendeleza mitindo mwafaka kwa ajili ya mwingiliano na uratibu kati ya wadau mbalimbali katika mfumo wa kifedha.


• Kuimarisha uwezo kwa ajili ya biashara ya maeneo: Kufanya biashara ya bidhaa iwe ya kieneo na kuleta upatanifu kati ya mifumo ya biashara. Kuondoa vikwazo vya biashara kati ya nchi na kupana ujuzi na taarifa za soko kati ya nchi.


• Kufanya uvumbuzi katika mifuatano ya vyakula maarufu vya maeneo: Kuhimiza jumuiya za kiuchumi za kieneo ili kuendeleza mipango inayoshughulikia vikwazo vinavyozuia masoko ya maeneo yasifanye kazi vizuri, kama vile miundo msingi, usafirishaji na ufisadi.


• Mazungumzo tendaji na sekta ya kibinafsi na kamati teule za bunge: Sekta ya kibinafsi na wabunge kutoka serikali za nchi za Afrika lazima wafanye kazi pamoja bila upendeleo wowote ili waharakishe uwekezaji wa serikali katika kilimo na kuanzisha sera na kanuni zinazochochea sekta ya kibinafsi iwekeze katika kilimo.


Taarifa kamili ya AGRF itatolewa mapema mwaka wa 2013.


Distributed by the African Press Organization on behalf of the African Green Revolution Forum (AGRF).


Wasiliana na - Deanna Petersen, +27 29 702 8033 or [email protected]


Kuhusu AGRF (@agrforum; #AGRF2012)

The African Green Revolution Forum (AGRF) (http://www.agrforum.com) inasisitiza ukuzaji wa uwekezaji na kusaidia sera za kuedeleza mazao ya kilimo na ukuaji wa mapato kwa wakulima wa Kiafrika katika njia inayo endeleza mazingira. Baraza hili ni juhudi inayo ongozwa na sekta ya kibnafsi iletayo wadao mbali mbali pamoja kujadili na kuendeleza mipango dhabiti ya wekezaji ili kufanikisha Uboreshaji wa Kilimo katika Afrika. Washirika wa kuu muhimu ni Pamoja na AGRA (http://www.agra-alliance.org), Yara International (http://www.yara.com), the Africa Union (http://www.au.int) na wakala wa mipango na uratibu wa NEPAD (http://www.nepad.org).